Tambwe alisajiliwa kwa dau la milioni 34, na kupewa mshahara wa milioni 3.4 ikiwa ni mara mbili zaidi ya ilivyokuwa Simba

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga Amis Tambwe huenda mambo yake yakawa mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa Simba kutokana na mshahara mkubwa anaopewa na vijana hao wa Jangwani ambao ni mara mbili na ule aliokuwa analipwa Simba.
Tambwe aliyejiunga na Yanga masaa machache kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu ya wiki hii alipokuwa SImba alikuwa akilipwa mshahara wa Milioni 1.7, na mara baada ya kutemwa na Simba aliyoifungia mabao 19 msimu uliopita na kuchukuliwa na Yanga kwa dau la milioni 34, na kupewa mshahara wa milioni 3.4 ikiwa ni mara mbili zaidi ya ilivyokuwa Simba.
“Amis Tambwe, ameiambia Goal anajisikia furaha sana kutua Yanga na kutokana na kiwango hicho cha mshahara atahakikisha anapambana na kuipa timu hiyo mafanikio ikiwemo kufunga mabao mengi zaidi ya ilivyokuwa Simba,”amesema Tambwe
Tambwe ametemwa na Simba baada ya klabu hiyo kuwasajili wachezaji wawili raia wa Uganda Danny Serunkuma kutoka Gor Mahia ya Kenya na Simon Sserunkuma aliyekuwa akiichezea timu ya Victoria University ya Kampala Uganda.
No comments:
Post a Comment