MABINGWA Tanzania Bara, Azam FC wamerejea nchini wakitokea nchini Uganda walipopiga kambi ya siku 10 kujianda na pambano la Jumapili dhidi ya Yanga Goal inafahamu.

Azam iliyopo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi wamepania kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini yao ya kutetea ubingwa wao msimu huu.
Lakini wakati timu hiyo ikijiandaa kwa pambano hilo Shirikisho la soka Afrika CAF , limetoa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Azam imepangwa kuanza na El Merreikh ya Sudan.
Hiyo ni mara ya kwanza Azam kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Taarifa ya Caf inaonyesha Azam FC itaanzia nyumbani Dar es Salaam na kumalizia ugenini Kharthoum.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili Julai 2014 timu hizo zilikutana Kigali Rwanda kwenye michuano ya Kombe la Kagame na El Marreikh, ikashinda kwa penalt 5-4, ukiwa ni mchezo wa nusu fainali.
Endapo Azam itafanikiwa kulipa kisasi na kuitoa El Marreikh itapambana na Lydia Ludic B.A ya Burundi au Kabuscorp do Palanca ya Angola.
No comments:
Post a Comment