Saturday, 27 December 2014

Pluijm aomba siku saba kuibadili Yanga


Kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba ili kukibadilisha kikosi hicho ili kiweze kucheza soka la kuvutia kama ilivyokuwa siku za nyuma

BAADA ya kupewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kukinoa kikosi cha Yanga kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba ili kukibadilisha kikosi hicho ili kiweze kucheza soka la kuvutia kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Pluijm aliyechukua mikoba ya Mbrazili Marcio Maximo ameiambia Goal kuwa amepania kutoa mbinu zake zote kwa klabu hiyo kutokana na uaminifu mkubwa alioonyeshwa na viongozi wa Yanga hata kumchagua kumrudisha yeye kukinoa kikosi chao.
Pluijm aomba siku saba kuibadili Yanga
“Yanga ni klabu kubwa yenye uwezo wa kumuajiri kocha yeyote inayo muhitaji bila kujali anatoka bara gani lakini anafurahi kupewa nafasi ya pekee kurudi kuifundisha timu hiyo kwa mara ya pili baada ya ile ya awali na kuifanya timu hiyo kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita,”amesema Maximo.

Pluijm tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi chake akishirikiana na kocha Charles Boniface Mkwasa na kibarua chao cha kwanza itakuwa Desemba 28 wakati timu hiyo itakapo kabiliana na mabingwa watetezi Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment