Tuesday, 30 December 2014

Simba yamtema Phiri, nafasi kuzibwa na Mserbia Goran Kopunovic


Simba yamtema Phiri, nafasi kuzibwa na Mserbia Goran Kopunovic 
 
KLABU ya Simba imekuwa timu ya tatu msimu huu kumtimua kocha wake Patrick Phiri
KLABU ya Simba imekuwa timu ya tatu msimu huu kumtimua kocha wake Patrick Phiri baada ya Ndanda FC na Yanga kufanya hivyo wiki iliyopita.
Rais wa Simba Evanse Aveva ameiambia Goal kuwa nafasi ya Phiri itachukuliwa na Goran Kopunovic, raia wa Serbia atakaye wasili Tanzania kesho Jumatano kwa ajili ya kusaini mkataba.
Aveva amesema wameamua kuachana na Phiri baada ya Mzambia huy kushindwa kuipa mafanikio timu hiyo katika kipindi cha miezi minne alichokuwa akiifundisha baada ya kumtimua Mcroatia Zdravko Logarusic.
“Tunamshukuru kwa kipindi chote alichokuwa na sisi tunajua yeye ni kocha mwenye rekodi nzuri na sisi siku za nyuma lakini safari hii ni mazi mambo yamekuwa magumu kwake kutokana na soka la Tanzania kuwa na ushindani mkubwa tunamtakia kila la kheri aendapo,”amesema Aveva.
Goran Kopunovic atakaye kuwa Mserbia wa pili kuifundisha Simba baada ya Milovan Cirkovic, aliwahi kufanya kazi nchini Rwanda katika timu ya Polisi na kuipa mafanikio kabla ya kutimkia Vietnam.

No comments:

Post a Comment