BAADA ya kutemwa kwenye dirisha dogo la usajili na klabu ya Yanga, Hamisi Kiiza ameiambia Goal anamsubiri wakala wake ili amwambie timu gani atajiunga nayo baada ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali zikiwemo za ndani na nje ya Uganda.
Hamisi Kiiza nafasi yake imezibwa na Mrundi Amisi Tambwe, aliyekuwa Simba alisema viongozi wa Yanga hawakumtendea haki kwa kumuacha siku ya mwisho huku dirisha la usajili likiwa limeshafungwa.
“Nikweli sikuwa na mahusiano mazuri na kocha Marcio Maximo, lakini baada ya kuwepo taarifa kuwa atatimuliwa nikahakikishiwa kuwa ntabaki ndani ya klabu kwakua anarudishwa kocha Hans van der Pluijm na anakubali uwezo wangu lakini siku ya mwisho nikashangaa nakabidhiwa barua ya kuachwa,”amesema Kiiza.
Kiiza alijiunga na Yanga mwaka 2011, akitokea URA ya kwao Uganda ameisaidia timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara mara moja ubingwa wa kombe la Kagame mara mbili na Ngao ya Jamii mara mbili.
No comments:
Post a Comment