KLABU ya Simba imemuongeza mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wake raia wa Uganda Emanuel Okwi, baada ya ule wa miezi sita kukaribia kumalizika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uteandaji ya Simba SC, Zacharia Hanspope ameiambia Goal kuwa wameamua kumwongeza mkataba Emmanuel Okwi, baada ya kuridhishwa na mchango wake anaoutoa kwenye timu hiyo tangu alipojiunga nayo Agosti 2014.
“Okwi ni mchezaji mzuri, amekuwa na mchango mkubwa kwa Simba hivyo hatuna budi kumuongezea mkataba ili aendelee kuwa nasi na kupata matunda yake,” amesema Hanspope.
Okwi alijiunga na Simba SC kwa mkataba mfupi wa miezi sita Agosti mwaka huu ili kulinda kiwango chake wakati akiendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili dhidi ya Yanga SC. Mganda huyo alishinda kesi hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha kwamba mkataba wake na Yanga SC ulikuwa umevunjwa.
No comments:
Post a Comment