Saturday, 3 January 2015

Nidhamu ndiyo mafanikio|”- Goran Kopunovic

“Nidhamu ndiyo mafanikio|”- Goran Kopunovic
Kopunovic raia wa Serbia ameahidi hatokuwa na mzaha hata kidogo


KOCHA wa Simba, Goran Kopunovic amewataka wachezaji wa timu hiyo kuzingatia nidhamu muda wote ili waweze kufanikiwa malengo yao waliyojiwekea.

Kopunovic raia wa Serbia ameiambia Goal hatokuwa na mzaha hata kidogo kwasababu lengo lake ni kuwa na timu bora inayocheza soka la kuvutia uwanjani lakini pia nidhamu ambayo itakuwa nikitu cha kuzingatia.

“Sitaki kuwatisha lakini hili nilisemalo la nidhamu ndiyo mafanikio yakila siku sitopenda kuona wachezaji wangu wakipewa kadi za kizembe na kuiumiza timu wakati mashabiki na viongozi wanaumia,”amesema Kopunovic.

Mserbia huyo ametua Tanzania jana asubuhi kuchukua nafasi ya Patrick Phiri aliyetimuliwa kazi baada ya kushindwa kuiongoza vyema timu hiyo tangu alipojiunga nayo Julai 2014.

No comments:

Post a Comment