
Yanga imepangwa kundi B, la michuano hiyo inayoshirikisha timu 12 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
Kocha Hans van der Pluijm, wa Yanga amesema amepanga kuwatumia wachezaji wengi chipukizi kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo inaanza leo kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Pluijm ameiambia Goal kuwa ina idadi kubwa ya wachezaji na wote wanalazimika kucheza kwa kupeana zamu ili kuipa nguvu timu hiyo iweze kumudu ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa watakayo shiriki mwezi ujao.
“Michuano hii nataka kuwatumia zaidi wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye mechi za Ligi Kuu lengo langu ni kila mmoja apate nafasi ya kucheza ili apandishe kiwango chake na siyo kukaa benchi,”amesema Pluijm.
Yanga imepangwa kundi B, la michuano hiyo inayoshirikisha timu 12 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment