Mashabiki wengi wameonekana kuipa nafasi kubwa Ivory Coast wakidai ni timu ambayo inawachezaji wengi wanaofanya vizuri hususani katika ligi za Ulaya
IKIWA yamebakia masaa machache kabla ya michuano ya Mataifa ya Afrika kuanza kutimua vumbi nchini Equatorial Guinea, mashabiki kutoka mataifa mbalimbali hususa yale ambayo hayakupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo wameanza kutafuta timu za kushangilia.
Watanzania nimiongoni mwa mashabiki ambao wamejipa uraia wa mataifa 16 wakijichagulia timu za kushangilia baada ya timu yao ya Taifa ‘Taifa Stars’ kushindwa kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo .
Mtandao wa Goal umekuwa ukizungumza na mashabiki mbalimbali wa soka Tanzania kuwahoji kuhusu fainali hizo ambazo zinafanyika Equatorial Guinea, na ni timu gani ambayo wanaipa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo baada ya bingwa Mtetezi kushindwa kufuzu.
Wengi wa Tanzania wameonekana kuipa nafasi kubwa Ivory Coast wakidai ni timu ambayo inawachezaji wengi wanaofanya vizuri hususa katika ligi za Ulaya na kutokuwepo kwa Nigeria na Egypt kunaweza kuwapa sababu ya wao kuchukua ubingwao huo.
Kitu kingine ambacho mashabiki hao wamesema kinaweza kuwa chachu ya Ivory Coast kuwa bingwa ni kiungo wake Yaya Toure, kuchaguliwa mchezaji bora wa Afrika mara nne mfululizo kitu ambacho kitawapa hamasa wachezaji wa timu hiyo waweze kujituma na kuchukua ubingwa huo mwaka huu.
“Naishabikia Ivory Coast kwa sababu ni timu ambayo inamasataa wengi wanacheza soka la kuvutia na nitimu ambayo ipo pamoja kwa muda mrefu na inaundwa nawachezaji wengi wenye umri mdogo wanaocheza Ulaya,”amesema Ali Makame mmoja wa mashabiki.
Shabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Kayeke, ameiambia Goal kuwa sababu ya kuipa nafasi Ivory Coast, ni kutokana na jitihada za Serikali ya nchi hiyo kuupa mchezo wa soka kipaumbele kwa kujenga vituo mbalimbali vya soka ambavyo vimekuwa vikiibua wachezaji kila siku.
Kayeke amesema kitu kingine ambacho kitakuwa chachu ya Ivory Coast, kuchukua ubingwa wa mwaka huu ni baada ya kutolewa katika hatua ya robo fainali katika fainali zilizo pita nchini Afrika Kusini na pia kufungwa kwa penati na Zambia katika fainali za mwaka 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon.
“Matumaini kubwa kwa timu yangu ni uwepo wa kocha HervĂ© Renard aliyeipa ubingwa Zambia mwaka 2012 ni kocha anayelijua vizuri soka la Afrika kwahiyo naamini anaweza kuwatumia vizuri wachezaji aliokuwa nao na kuipa ubingwa Ivory Coast mwaka huu,”amesema shabiki huyo.
Pamoja na kwamba michuano hiyo imekosa msisimko kama ilivyokuwa zamani lakini niwazi kuwa faianli za mwaka huu zimevuta hisi za mashabiki wengi wa soka duniani kote kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni klabu za Ulaya kutafuta wachezaji wa kununua kwa ajili ya kuziimarisha timu zao.
Pamoja na Ivory Coast kupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu lakini haitakuwa rahisi kama ambavyo mashabiki wake wanadhani kutokana na timu ambazo imepangwa nazo kundi moja la D lenye timu za Mali,Mali, Guinea na wapinzani wao Cameroon ambapo katika mchezo wa awali kwenye kuwania kufuzu fainali hizo walikuwa kundi moja la D na Cameroon WALIIFUNGA Ivory Coast mabao 4-1, pambano likichezwa kwenye uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
No comments:
Post a Comment